Zaidi ya Shillingi Millioni 200 na 15 wamekebidhiwa wananchi wa Jozani kwa maendeleo ya vijiji vya hifadhi ya jozani .

Wananchi wa kusini unguja wamesema licha ya  serikali  kufanya juhudi  za kulinda misitu  katika hifadhi mbalimbali ikiwemo Jozani na Ghuba chwaka  lakini bado kuna baadhi ya watu wanafanya hujuma katika maeneo hayo.
Akisoma risala ya wanakijiji  wa Jozani, wakati wa mgao wa Fedha wa hifadhi ya misitu   Mussa Saleh Mihambo amesema takribani miaka 16 
wanakijiji wanamefaika kupitia msitu huo katika hivi sasa kumejitokeza  watu kuuhujumu msitu kwa kufanya vitendo vya uwindaji  holela wa wanyama  na ukataji wa miti,Uvamizi  wa maeneo  ya misitu  kwa kisingizio cha kuimarisha kilimo,Ujenzi holela  wa nyumba za makaazi  unaosababisha  uharifu wa misitu na yote hayo yamesababishwa na ulinzi duni wa msitu wa hifadhi ya taifa jozani.
Nae Mkuu wa wilaya ya Kati Mashavu Sukwa amesema nikweli msitu  unaharibiwa  na kukatwa kwa  kasi kubwa  katika maeneo hayo na kusababisha  uharibifu wa mazingira na kupelekea kushuka kwa pato la taifa hivyo amesema ili kunusuru hali hiyo nivyema  katika maeneo hayo ya misitu kufungwe nyuki  ili kunusuru hali hiyo kwalengo la kuuhigfadhi.
Kwaupande wake Waziri wa kilimo Mali asili mifugo na uvuvi Hamad  Rashid  Mohamed amesema kutokana na matatizo hayo Serikali ya Mapinduzi zanzibar itachukua hatua  za kisheria  kwa  kuwafikisha  watenda  hujuma katika vyombo vya sheria ili  kudhibiti  rasilimali hizo ambazo zinaingiza pato la taifa kupitia  Fedha za kigeni.
Aidha amesema chanzo cha matatizo hayo yote ni wanajamii kutokuwa na utayari kushirikiana na serikali katika hatua mbalimbali za maendeleo  kwa kuwafichua wahalifu na badala yake huendekeza Muhali na  kupelekea  athari kubwa katika hifadhi.
Zaidi  ya Shillingi Million 200 na 15   wamekebidhiwa  wananchi  wa Jozani  kwa maendeleo ya vijiji vya hifadhi ya jozani  kwa lengo la  kubuni miaradi ya maendeleo.
chanzo:ZANZIBAR24

Comments