
Jana jioni Mfanyabiashara huyo alichukuliwa na gari la kubebea Wagonjwa lenye namba za usajili za DFP na alionekana akitembea na kuingia kwenye gari hilo (Land Cruise Nyeupe) yeye mwenyewe bila kubebwa au kusaidiwa huku gari lake aina ya Range Rover likitangulia mbele na watu wengine.
Baada ya gari hilo kumchukua msafara huo ulikwenda moja kwa moja kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Muhimbili Dar es salaam ambako watu mbalimbali wanaosumbuliwa na moyo hupata matibabu.
Gari la wagonjwa lililombeba Yusuf Manji na gari lake binafsi katika viunga vya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
chanzo:mpekuziblog.
Comments