Waziri wa mambo ya nje wa Marekani
Rex Tillerson amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Mexico Luis
Videgaray mjini Mexico, mkutano ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na
masuala ya sera za uhamiaji.
katika mkutano huo, Waziri wa mambo
ya nje wa Mexico, Luis Videgaray, ameonyesha kuchukizwa kwake na Sera za
Marekani dhidi ya nchi yake.
Amemueleza US Secretary of state,
Rex Tillerson na mkuu wa masuala ya usalama , John Kelly kuwa
mapendekezo ya marekani kuhusu masuala ya uhamiaji yana madhara.
Alikua akikosoa mpango wa Marekani kuwarejesha makwao wahamiaji waishio Marekani bila vibali bila kujali raia wa Mexico au la.
''ni
heshima kubwa na tunatoa shukrani kwa ujio huu, kwa kuwa umefanyika
kipindi kigumu kwa Mexico na Marekani.kama nyote mjuavyo, kumekuwa na
hali ya kutoridhishwa ,hali ya kukerwa na kile kinachoelezwa kuwa sera
ambazo zinaweza kuleta athari kwa maslahi ya raia wa Mexico ndani na nje
ya Mexico''
Kwa upande wake bwana Kelly amesema hakutakuwa na
zoezi la kuwarejesha makwao raia wa kigeni waishio kinyume cha sheria
nchini Marekani na kuwa jeshi halitatumika kwenye operesheni ya
kuwarudisha nyumbani.Amesema hatua zote zitachukuliwa kwa kufuata Sheria.
Naye
Rais wa zamani wa Mexico, Vicente Fox ameonyesha wasiwasi wake kuhusu
utawala wa Trump kuwa umeharibu mahusiano mazuri yaliyokuwapo kati ya
Mexico na Marekani.
Maafisa hao wawili pia walikutana na Rais wa
Mexico, Enrique Pena Nieto, ambaye hivi karibuni alisitisha safari yake
ya kukutana na rais wa Marekani,Donald Trump, baada ya Trump kusisitiza
kuwa Mexico ilipe gharama za kujenga ukuta wa mpaka baina ya Marekani na
Mexico.
chanzo:Bbc.
Comments