Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imezitaka pande zote mbili
zinazohusika katika kesi hiyo namba 311 ya mwaka 2016 kufanya usuluhishi
kabla ya kusikilizwa.
Mwakilishi wa Wizara ya Elimu, Anna Kalomo amedai mbele ya Jaji Rose
Temba kuwa ili kutoa uamuzi mzuri katika shauri hilo ni lazima Waziri
husika awepo kwa kuwa tayari viongozi wengine wametoa mwongozo hivyo
anasubiriwa Waziri.
Hata hivyo, aliomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi tarehe
nyingine kwa ajili ya kumpatia muda Waziri kupitia shauri hilo na kutoa
mwongozo.
Jaji Rose Feleshi aliahirisha kutolewa kwa uamuzi huo hadi Februari
15 mwaka huu kwa ajili ya kupokea mwongozo wa Profesa Ndalichako ili
kesi hiyo ianze kusikilizwa kwa Jaji Elieza Feleshi.
Mbali na mwakilishi huyo wa Wizara, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU),
inawakilishwa na Wakili Rose Ruta, Wakili wa Chuo hicho ni Jerome Msemwa
na Wakili wa wanafunzi hao, Emmanuel Muga.
Madai ya msingi katika kesi hiyo inadaiwa kuwa walalamikaji
(wanafunzi) hao wanadai fidia ya miaka mitatu waliokaa chuoni hapo dhidi
ya TCU na chuo hicho cha Mtakatifu Joseph.
Awali wakati wa kufungua kesi hiyo, wanafunzi hao waliwasilisha
maombi kupitia wakili Muga wakiomba kibali cha kuwawakilisha wenzao
mahakamani hapo pamoja na kusitisha masomo wakati kesi ya msingi
ikiendelea kusikilizwa.
Muga alidai kuwa wanafunzi ambao watawawakilisha wenzao ni Innocent Peter, Ramadhan Kipenya, Oswald Mwinuka na Feith Kyando.
Uamuzi wa wanafunzi hao kukimbilia mahakamani unatokana na agizo la
Waziri huyo, Joyce Ndalichako lililoeleza kuwa kutokana na tatizo la
ufundishaji wa Stashahada ya Elimu (Sayansi, Hisabati na Teknolojia)
wanafunzi wote wanaosomea elimu hiyo wanatakiwa kurejea nyumbani.
chanzo:zanzibar24.
Comments