Tukio hilo la kusikitisha limetokea Tasani Makunduchi wilaya ya
kusini Unguja wazee hao waliofahamikwa kwa jina la Ramadhan Issa Simai
(55) na mwenziwe Ali Suleimani Ameir (43) wote wakaazi wa Tasani
Makunduchi ambapo walimbaka kwa zamu mtoto huyo na kumsababishia maumivu
makali.
Nae mzazi wa mtoto huyo amesema mmoja wa wazee hao alifika nyumbani
na kumpa pesa mtoto huyo kumbe ndio mtego wa kumfanyia unyama huo na
kusema kuwa hana ujamaa na waliomharibia mwanawe hivyo hatua kali za
kisheria zichukuliwe zidi yao.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi kamishna
msaidi wa polisi Juma Saadi Khamis amelaani kitendo hicho na kusema kuwa
wazee hao tayari wameshatiwa mikononi mwa polisi kwa kuchukuliwa hatua
za kisheria.
chanzo: zanzibar24.
Comments