
Akizungumza katika kikao maalumu na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya
pamoja na Makamanda wa Jeshi la polisi amesema kuna baadhi ya viongozi
hawasimamii vyema sheria katika kufanya kazi na badala yake kufanya
kazi kwa maslahi yao binafsi.
Hivyo amewataka wakuu hao , jeshi la polisi pamoja na Masheha
kuzingatia utaratibu uliowekwa na serikali katika utoaji vibali
ili serikali iweze kunufaika na mapato pia kuzidisha ulinzi katika
maeneo
yanayochimbwa mchanga na yale maeneo yasio rasmi kuchimbwa.
Kwa upande wao Wakuu wa Mikoa Mitatu ya Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud,
Dk. Idrisa Muslih Hija na Vuai Mwinyi wamesema kutokana na janga hilo
hawatamfumbia mtu macho katika kudhibiti uchumbwaji mchanga hasa wale
wanaochimba kinyume na sheria bila ya kibali maalum kutoka serikalini.
Kikao hicho kilichowakutanisha Waziri wa kilimo, MaDC wa mikoa yote
unguja, MaRC pamoja na Jeshi la polisi kinalengo la kutafuta njia za
kudhibiti rasilimali hiyo kutotoweka hapa zanzibar.
CHANZO:Zanzibar24 .
Comments