Wajumbe wa baraza la wawakilishi waililia sekta ya elimu Zanzibar.

baraza-la-wawakilishiWajumbe wa Baraza la wawakilishi wameiomba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kuyamalizia Majengo ya Skuli yalioanza kujengwa na wananchi  ili wanafuzi waweze kusoma katika mazingira salama kutokana na baadhi ya majengo hayo kuwa hatarini kuanguka.
Wakiuliza maswali ya nyongeza katika mkutano wa Baraza wawakilishi huko chukwani nje kidogo ya Manispaa ya mji wa Zanzibar wajumbe hao wamesema mbali
na jitihada za wananchi katika kusaidia sekta ya elimu jitihada zao hazifikii malengo kutokana na kukosa ushirikiano mzuri wa serikali.
Aidha wamesema skuli mbali mbali zimekuwa na matatizo ya Uchakavu wa majengo hususani katika Mapaa jambo ambalo linapelekea wanafunzi kutumia madarasa machache ili kulinda usalama wa afya zao wakati wakiendelea na masomo na baadhi ya skuli wanafunzi  kusoma chini ya miti ikiwemo skuli ya Mgambo.
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri amesema wizara inaendelea na jitihada  mbalimbali za kujenga skuli hizo kwa awamu pamoja na kuendelea kuezeka skuli ambazo zimejengwa na wananchi.
Aidha amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na wadau wa maendelo wakiwemo Zanzibar foundation watahakikisha wanayapatia ufumbuzi matatizo yote yanayoikumba sekta ya elimu ili wanafuzi waweze kupata elimu katika hali nzuri.
Jumla ya madarasa 31 unguja na madarasa 30 pemba yameshakamilishwa kujengwa na Milele Zanzibar Foundation ambapo jumla ya madarasa  285 yakiwemo ya skuli ya mgambo yapo katika mkakati wa kuezekwa.
chanzo:zanzibar24.

Comments