Sheria iliyobuniwa miaka mitano iliyopita ina walazimu wanaume
au wanawake kupokea mshahara wa zaidi ya dola elfu ishirini na tatu, kabla ya
kukubaliwa kuwaalika wachumba wao ambao ni raia wa kigeni.
Hata hivyo sheria hiyo haiwahusu raia wengi wa mataifa ya Ulaya.
Majaji wamesema kuwa sheria hizo zilikuwa na malengo ya kisheria
ingawa haiwajali watoto wanaohusika katika ndoa za aina hiyo.
Lord Carnwath,mmoja wa majaji waliotoa hukumu hiyo amesema
sheria juu ya kipato cha chini inalenga kuhakikisha wanandoa hashawishiwi na
mkumbo wa kukimbilia faida ya ustawi na kuwa na rasilimali za kutosha
kugharamia maisha yao nchini Uingereza.
Kwa upande wake Saira Grant,amesema familia za raia wa Uingereza
zinavunjwa kwa sababu ya kizuizi kilichobuniwa na binadamu.
Comments