Kundi hilo lilikuwa linakabiliana na kundi jingine la raia wa Afrika kusini wanaoongoza ghasia dhidi ya wahamiaji.
Hatahivyo maafisa wa polisi waliingilia kati na kuwatimua kwa kutumia ndege aina ya helikopta pamoja na risasi za mipira.
Takriban watu wawili wamejeruhiwa na risasi hizo za mipira wakati
polisi walipokuwa wakitawanya maandamano dhidi ya wageni nchini humo.
Maafisa
wa polisi wametumia ndege aina ya helikopta ,risasi za mipira na vitoa
machozi kuwatawanya waandamanaji hao kuzuia makundi ya wahamiaji
yaliojitokeza yaliojihami na fimbo,mawe na visu.
Wanaharakti wa shirika la Save South Afrika wanasema kuwa Meya wa Johannesburg Herman Mashaba ana maswali mengi ya kujibu.
chanzo:Bbc.
Comments