
Hafla ya makabidhiano hayo, yalifanyika kwenye mabanda ya kufugia
Ng’ombe hao yanayomilikiwa na kikundi cha Umoja ni nguvu cha shehia
hiyo.
Mradi huo wa kopa Ng’ombe lipa Ng’ombe, uliochini ya Mradi wa
kuimarisha huduma za kilimo na mifugo ASSP na ASDP-L unaodhaminiwa na
Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo ‘IFAD’ kupitia serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikundi cha umoja ni nguvu kilikabidhiwa Ng’ombe 20 mwaka 2015 wakiwa
na mimba, lengo baada ya kuzaa majike ni kuwapatia wananchi wenzao
ndama hao, ili nao wanufaike na mradi huo.
Akizungumza kabla ya ugawaji wa Ng’ombe hao saba kutoka kwa
wanakikundi cha Umoja ni nguvu kwenda kwa wanakikundi wengine, Mratibu
wa mradi huo wa ASSP-ASDP-L Pemba Asha Omar Faki, alisema lengo ni kuona
Ng’ombe hao wanasambaa kwa wananchi wote.
Mratibu huyo alisema, miongoni mwa masharti ya mradi huo ni kuwa
wananchi wafugaji kujikusanya pamoja, ili kuendesha ufugaji na kisha
wanapozaliwa wengine kuwagawa kwa wengine.
“Huu mradi lengo lake ni kuona unasambaa kwa jamii yote, baada ya
wanaokabidhiwa Ng’ombe awali wakishazaa, hutakiwa kuwapa wengine ili nao
wafuge na baada kuwapatia wengine kama tunavyofanya leo’’,alifafanua.
Kwa upande wake mjumbe wa kikundi cha umoja ni nguvu kilichotoa
Ng’ombe (ndama) saba, Said Juma Salim alisema waliyalea makoo hayo 20,
waliokabidhiwa ingawa wanne walikufa baadae.
“Haya makoo 16 yaliobakia yameshazaa, na leo (jana) tunakabidhi ndama
majike saba, kwa wenzetu wafugaji ili nao wakafuge na kisha kuwapa
wenzao’’,alifafanua.
Akizungumza kwa niaba ya wafugaji wenzake wapya waliokabidhiwa ndama
hao, Salama Abdalla Mohamed alisema, watahakikisha wanawatunza na baada
ya kuzaa kuwagawa kwa wenzao wengine.
“Sisi tulikuwa na hamu ya kukabidhiwa ndama hawa, maana ufugaji
unaweza kututoa kwenye umaskini nzito tulionao sasa’’,alifafanua.
Mkuu wa Idara ya Mifugo Pemba Aisha Zaharan Mohamed alisema, wanavyo
vituo tisa kisiwani Pemba ambavyo vimeanzishwa na serikali, kwa ajili ya
wananchi ili kujiunga kwenye mpango huo wa kopa Ng’ombe lipa Ng’ombe.
Miongoni mwa vituo hivyo ni Makundeni, Vikunguni, Mizingani, Piki,
Kisiwani, Wingwi na Makangale ambapo wanavikundi hao, walikabidhiwa
Ng’ombe hao tokea mwaka 2015.
chanzo:zanzibar24
Comments