Akitoa neno la shukran mara baada ya chakula alichowaandalia vijana walioshiriki katika halaiki kwenye sherehe za maadhimisho Ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika hafla iliyofanyika huko katika viwanja vya vya Makao Makuu ya KVZ kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu alisema ni vyema kwa vijana kuendelea kuwa na mbegu za kizalendo ili kuendelea kunawirisha dhama ya Mapinduzi kwa miaka mingi zaidi ijayo.
Alisema ushiriki wa vijana hao uliojaa furaha katika sherehe hizo umeendelea kumpa moyo na matumaini makubwa Dk. Shein na hivyo anaamini kuwa kutaendelea ya kujenga hamasa kwa kushiriki kwa wingi zaidi katika sherehe zijazo zinapofikia za kusherehekea Mapinduzi ya Zanzibar kwa miaka ijayo.
Hata hivyo Dk. Shein alitoa pongezi maalum kwa vijana hao wa halaiki na makundi mengine yaliyoweza kushiriki vyema na kufanikisha sherehe hizo ambazo zilikuwa kubwa na za aina yake.
Mapema Katibu wa uhamasishaji wa Halaiki Ali Mohamed Baraka SHASHA amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed kwa kuendeleza utaratibu wa kuyakutanisha makundi mbali mbali kwa ajili ya kupongezana kutokana na kazi nzuri zinazofanyika katika sherehe hizo..
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Katibu Mkuu Kiongozi Abdulhamid Yahya Mzee, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, na viongozi wengine wa serikali.
chanzo:zanzibar24.
Comments