UN yazishukuru nchi jirani na Libya.

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amezishukuru nchi jirani na Libya kwa jitihada zao za kutafuta suluhisho la mgogoro wa ndani wa nchi hiyo.

Martin Kobler amezishukuru nchi za Misri, Tunisia na Algeria na kusema: Nchi jirani na Libya zimekuwa na mchango muhimu katika kupatanisha kati ya makundi hasimu nchini humo.

Jumatatu iliyopita Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Tunisia na Algeria walikutana nchini Tunisia kwa ajili ya kudumisha juhudi za kusitisha mapigano kikamilifu nchini Libya na kusisitiza udharura wa kufikiwa mapatano makundi yote ya nchi hiyo chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa. 
Mawaziri hao pia walisema kuwa hali ya maeneo ya mipaka ya nchi hizo na Libya inatia wasiwasi.
Libya imekuwa uwanja wa makundi ya kitakfiri na kiwahabi ambayo yanatumia mipaka ya nchi hiyo kupeleka nje magaidi na wahamiaji haramu kuelekea nchi za Ulaya na Mashariki ya Kati.
chanzo:parstoday.

Comments