UKAWA watakiwa kuimarisha umoja.

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya Chama cha wananchi CUF imevishauri Vyama vinavyounga umoja wa Vyama vya UKAWA kuimarisha ushirikiano ili kuhakikisha vinapata nafasi za viongozi katika serikali na majimbo kwa lengo la kuleta maendeleo yanayohitajika katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi wa kata za Tanzania Bara uliofanyika tarehe 22/1/2017 na Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani Zanzibar huko katika ofisi za Chama hicho Vuga Naibu Katibu Mkuu Tanzania bara Joran Lwehabura Bashange amesema pindipo umoja wa UKAWA utakuwa pamoja katika kufutilia na kusimamia haki zao kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta maendeleo katika chama hicho.
Hata amesema wamedai kuwa matokeo mbali mbali ya Uchaguzi yanaonesha wazi kuwa chama cha CUF kina matokeo mazuri yaliotokana na nguvu za wananchi lakini kinarejeshwa nyumba na baadhi ya Viongozi kutotekeleza wajibu wao katika kutenda haki za uchaguzi.
 chanzo:zanzibar24.

Comments