Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imetoa adhabu kali kwa vituo vinne
vya utangazaji kwa kukiuka maadili ya utangazaji kwa mujibu wa
sheria na kuvitaka viombe radhi siku tatu mfululizo kuanzia leo (Ijumaa)
kupitia taarifa ya habari.
Akitoa adhabu
hizo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valerie Msoka amesema vitio
hivyo vimepewa onyo kali ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kuomba radhi
wasikilizaji wake.
Amevitaja
vituo hivyo kuwa ni Star TV,Channel ten, Clouds FM na Times FM.
chanzo:Mwananchi.
Comments