Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba
tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa
sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV
mtandaoni.
“Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and postal
communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma
zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano,” imesema barua hiyo.
Wamiliki wa mitandao hiyo Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi na Abdallah
Mrisho wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati
hata kanuni zenyewe hazijawekwa.
Watatu hao walingana kwa pamoja kwenda kuonana na mkurugenzi wa TCRA
ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhisiwa kuendelea kutoa huduma hiyo
kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa.
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo.
“Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na
haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya
kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii,” alisema Ankal. Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.
Ayo TV, Michuzi TV na Global TV ambazo zina watazamaji wengi ndani
na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa TCRA kati ya
vituo mtandao takriban 51 vilivyopata barua hiyo.
chanzo:zanzibar24
Comments