Serikali yatakiwa kuwalipa posho mashahidi wanaotoa ushahidi mahakamani.

baraza-la-wawakilishiMwakilishi wa jimbo la mgogoni shehe Hamadi Matari amesema kutolipwa posho kwa wakati mashahidi wanaotoa ushahidi mahakamani kunapelekea kuzorota kwa kesi nyingi katika mahakama.
Akiuliza swali katika kikao cha baraza la wawakilishi alipotaka  kujua ni mashahidi wangapi ambao wanadai posho zao na ni lini serikali itawalipa posho hilo
amesema mashahidi ni sehemu muhimu katika kesi lakini kumekua na malalamiko makubwa  kwa mashahidi hao kudai posho lao kwa muda mrefu
Akijibu swali hilo naibu waziri wa nchi ofisi ya rais katiba sheria utumishi wa umma na utawala bora Hamis Juma Mwalimu amesema serekali inatambua umuhimu wa mashahidi katika uendeshaji wa kesi mahakamani hivyo inaendelea kuwalipa fedha  mashahidi hao kwa awamu kadri ya fedha itakavyoruhusu.
Jumla ya shilling million nne na laki tano zimetengwa kwa ajili ya kuwalipa mashahidi kupitia idara ya mahakama ambapo jumla ya mashahidi 53 wanadai posho zao kwa kipindi cha miezi mitatu.
chanzo:Zanzibar24.

Comments