Akizungumza katika Ziara maalumu na Waandishi wa habari katika
ukaguzi wa maeneo yaliyoathirika kwa kuchimbwa mchanga katika mashimo ya
mchanga huko Zingwezingwe Mkuu wa kitengo cha Maliasili zisizorejesheka
Ngwali Makame Haji amesema Serikali inatarajia kutumia mbinu mbadala
kwa matumizi ya ujenzi bila ya kutumia mchanga ilikupunguza uharibifu
wa mazingira na kupotea kwa rasilimali hiyo nchini.
Kwaupande wao Vijana wanaojishuhulisha na ajira za kuchimba mchana
Chales John na Hamad Zamani Hatibu wameiyomba serikali kuwatafutia
mbinu mbada itakayowawezesha wao kujiajiri wenyewe kwani endepo
uchumbwaji wa mchanga utazuiliwa kutasababisha vijana wengine kukosa
ajira na kujiingiza katika vitendo viovu ili kujitafutia riski kwa
mahitaji yao ya kila siku.
chanzo: zanzibar24.
Comments