Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge aliyasema hayo jana
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo
yatakayofanyika kesho Dar es Salaam ambayo yatahudhuriwa na washiriki
zaidi ya 600.
“Serikali kupitia wizara yetu itakuwa mwenyeji wa maadhimisho haya na
yameandaliwa kwa ushirikiano na Nile Basin Initiative (NBI) ambao
jukumu lao kubwa ni kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la Mto
Nile kwa niaba ya nchi wanachama zipatazo 10,” alisema Lwenge.
Lwenge alizitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda,
Burundi, Ethiopia, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
na Misri.
Alisema Mto Nile ni miongoni mwa mito mikubwa duniani wenye urefu wa
kilometa 6,695 unaoanzia Ziwa Victoria nchini na ni chanzo kikubwa cha
maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, viwandani, kilimo cha
umwagiliaji na kuzalisha umeme kwa wakazi wa nchi za bonde hilo.
Alisema kaulimbiu ya mwaka huu imelenga kuonesha umma umuhimu wa Mto
Nile katika kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa chakula, maji na
nishati ya umeme kwa jamii nzima na kuonesha muingiliano uliopo katika
sekta husika kwa lengo la kuondoa umaskini, kuboresha maisha ya jamii na
kuleta maendeleo endelevu.
Alisema maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza kesho saa 2:30 asubuhi
kwa maandamano yatakayoongozwa na Bendi ya Polisi kuanzia Viwanja vya
Mnazi Mmoja hadi Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) ambako
maonesho na ufunguzi rasmi utafanyika.
Alisema maadhimisho hayo yatashirikisha watu mbalimbali zikiwemo
sekta mbalimbali, taasisi za serikali, taasisi zisizo za kiserikali,
wadau wa maendeleo na watu mashuhuri.
chanzo:Habarileo.
Comments