Sakata la SUZA kudahili wanafunzi wasio na sifa, Prof Rai atupia lawama vyombo vya habari na TCU.

Kufuatia sakata la wanafunzi takriban 8000 kutangazwa kukosa sifa za kujiunga na vyuo vikuu Tanzania,   Chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar (suza), kupitia Makamu Mkuu wa chuo hicho Prof Idris Rai kimetoa taarifa ya kukanusha kudahili  wanafunzi feki 966 kupitia ukurasa wake wa Facebook  huku akivitupua lawama vyombo vya kwa kueneza habari zisizo sahihi.

Alisema kuwa usambaaji wa taarifa hizo kumekipelekea chuo cha SUZA kupata taaswira mbaya, hivyo aliitaka jamii kutokuamini taarifa hizo.


Taarifa kwa Umma !
Kuna habari zimezagaa kutoka kwenye mitandao ya kijamii na vyombo kadha vya habari kwamba SUZA ina wanafunzi 966 ambao hawana sifa za kujiunga na chuo kikuu kwa vigezo vya TCU!.

Napenda kuwaarifu kwamba hiyo taarifa sio sahihi (FAKE NEWS) !!.

Ikumbukwe kwamba wanafunzi wote Wa Ngazi ya shahada na kuendelea wanasailiwa na TCU. Wanafunzi walioorodheshwa kwa chuo cha SUZA pia wanadahikiwa na kuthibitishwa na TCU.

Kilichotokea ni TCU kupoteza taarifa za baadhi ya wanafunzi kwenye kumbukumbu zao ambazo awali walituagiza tuzithibitishe. Tukiwasilisha uthibitisho wa wanafuzi hao tarehe 25 Januari kwa njia ya barua pepe!.

Kwa mshangao tumepokea barua nyengine ya TCU tarehe 20 Februari ikitutaka tuthibitishe orodha hiyo ya wanafunzi tena bila ya kutujulisha kwamba walipokea taarifa tulowatumia mwezi iliopita au la! Tulipewa tarehe 28 Februari kuwasilisha taarifa hizo mpya.

Kilojitokeza hapa kwa mtazamo wetu:

– vyombo vya habari kutoa taarifa zisizo sahihi kwa Jamii
– TCU kutokuwa makini katika kutoa taarifa kwa jamii, na kutokuzingatia sensitivity ya taarifa ilozitoa wakati tayari imeziomba taasisi ziwasilishe taarifa husika. Taarifa ambazo TCU ilitakiwa iwe nazo.

Taarifa hizi ambazo sio sahihi zimepelekea Jamii kupata picha kwamba SUZA hakifuati tararibu za udahili wa wanafunzi, au wanadahili wanafunzi kienyeji. Napenda kuwahakikishia watanzania wote kwamba jambo hilo halina nafasi katika chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.

Zaidi ya hayo, SUZA hatuna haja ya kufanya hivyo kwani kila mwaka twapokea wanafunzi wengi wanaoomba

kujiunga na SUZA zaidi ya nafasi ambazo zipo. 

Hii inaonesha kwamba SUZA ni katika vyuo ambayo vinapendelewa sana na wanafunzi kujiunga kutokana na ubora wa elimu tunayotoa.

Kwa hiyo – tupige vita Fake News zenye lengo la kutupaka matope!!!
Shukran
chanzo:zanzibar24.

Comments