Polisi nchini Malaysia wamesema kuwa
wamefichua kemikali iliyotumika kumuuwa nduguye wa kambo, kiongozi wa
Korea Kaskazini, na kuitaja kuwa VX dawa ya neva. Sumu kali mno
inayotumika katika vita vya kemikali.
Kim Jong-nam, aliuwawa katika
shambulio hilo la sumu, kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur, mapema
juma lililopita.
Kamera za CCTV zinaonyesha wanawake wawili waliobeba vitu wakati Kim Jong nam alipokuwa akijiandaa kuingia ndani ya ndege.
Korea
kaskazini wiki iliyopita ilisema kuwa haitambui matokeo yeyote
yatakayotokana na uchunguzi wao na kutaka warejeshewe mwili.
chanzo:Bbc.
Comments