Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Mohd Hafidh alisema hayo
wakati alipokutana na uongozi wa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi pamoja
na wataalamu wengine kutathmini hali ya majengo mbalimbali yaliyopo
katika Mji Mkongwe wa Zanzibar.
Alisema baadhi ya majengo ya nyumba hizo ni zile zinazomilikiwa na Shirika la Nyumba la Serikali zilizokuwa nyumba za maendeleo.
“Tumefanya tathmini ya nyumba zilizopo katika hali mbaya ambapo
tumebaini zipo nyumba 26 zinahitaji ukarabati mkubwa ambapo tumeomba
Serikali kutoa jumla ya Sh bilioni tano kuzirudisha katika hali halisi
ya ubora wake,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud alisema
Serikali imeweka malengo na mikakati ya kuufanya mji wa Zanzibar ikiwemo
sehemu ya Mji Mkongwe kuwa kivutio cha watalii.
Alisema juhudi hizo ni pamoja na kuyafanyia ukarabati mkubwa majengo
yaliyopo Mji Mkongwe ambayo baadhi yake yapo katika hali mbaya ya
uchakavu kiasi ya kutishia maisha ya wananchi.
“Tumeweka mikakati ya kufanyia ukarabati mkubwa majengo yaliyopo
katika Mji Mkongwe na sehemu nyingine ili yawe kivutio kwa wageni,”
alisema.
chanzo:habarileo.
Comments