Mwakilishi wa uzini Mh Raza Awasisitiza Viongozi wa Serikali Kutekeleza Ahadi zao za Majimboni.

Viongozi wa Serikali wametakiwa  kutekeleza  ahadi walizotoa wakati wa kampeni  ili kuharakisha maendeleo ya wananchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mohammed Raza amesema baadhi ya viongozi wa serikali wamekuwa wanakwamisha maendeleo  kwa wananchi kutokana na kuchelewa kuwapelekea maendeleo  licha ya kuwa wakiahidi  wakati wa kampeni kuwa watawatumikia..
Hata hivyo amesema wakati umefika kwa viongozi  kutekeleza hadi kwa vitendo kwani wananchi wengi wenye vipato vya chini  hushindwa  kuzifikia  huduma za kijamii  kutokana na changamoto mbalimbali zinazotokana na hali  gumu ya maisha.
Aidha amestoa wito kwa serikali kuzielekeza nguvu zao kwenye Afya kwani wananchi  wanashindwa kumudu gharama za matibabu,na kwenye  Elimu  kutokana na wazazi wengi hushindwa kuwaendeleza watoto wao kutokana na  ugumu wa maisha  pamoja na kuwasaidia vijana masuala ya Ajira  ili kuweza kujiajiri wenyewe.
chanzo:zanzibar24.

Comments