
Kauli hiyo imetolewa na Mtakwimu mkuu wa serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Mayasa Mahafudhi Mwinyi, wakati akifungua semina ya siku
mbili, kwa wazalishaji na watumiaji wa takwimu kisiwani Pemba.
Alisema, anaeficha takwimu ni sawa kwamba anadumaza uchumi wa nchi na
hatimae kudhoofisha nguvu za serikali, katika kuelekea kwenye maendeleo
endelevu.
Alieleza kuwa, mipango na mikakati yote ya serikali inahitaji kuwa na
takwimu sahihi na zinazokwenda na wakati, hivyo iwapo kunataasisi
wanashindwa kuzitoa, huwa ni adui kwa uchumi nchi.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, hakuna linaloweza kufanyika iwe
kwenye ngazi ya serikali kuu, au familia pasi na kuwa na takwimu sahihi,
ambazo zinaweza kumpa mwanga kwa kile anachotaka kukifanya.
“Suala la kuficha au kupotosha takwimu kwa wanaotaka kuzitumia sio
jambo zuri, maana kila hatua ya kufikia maendeleo ndani ya nchi au mtu
mmoja mmoja, basi inahitaji takwimu sahihi’’,alifafanua.
Hata hivyo Mtakwimu huyo mkuu wa serikali, amewataka wanaohitaji
takwimu sahihi, wasisite kutumia ofisi yao, ili kuhakikisha wanapata
takwimu sahihi kwa kazi zao.
Akiwasilisha mada juu ya uzalishaji na umuhimu wa takwimu na matumizi
yake, Mtakwimu shek-sheni ya takwimu za huduma Mwanangaza Mataka
Hafidh alisema kukosekana kwa takwimu mfano za wageni wanaoingia nchini,
ni kosa ambalo linaweza kuigharimu idara husika.
“Ili takwimu halisi zipatikane, lazima kuwe na hatua kadhaa ikiwani
pamoja na maandalizi, uwekaji wa kumbukumbu na kufanyika kwa tathmini,
ili takwimu hizo ziwe na viwango na ubora unaotakiwa’’,alisema.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo walisema wakati umefika kwa
tawkimu husika zisambaazwe ili kila mmoja aweze kuzipata kwa urahisi.
Mohamed Najim kutoka mtandao wa asasi za kuraia Pemba, PACSO alisema
lazima kwa ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali, lazima iweke takwimu hizo
maana asasi za kiraia zimekuwa zikisumbuuka wanapozihstaji hasa
wanapoomba miradi kwa wafadhili.
Nae Salum Abdalla Salum kutoka UWZ Pemba, alisema bado jamii imekuwa
na hofu kushirikiana kikamilifu na watu wa takwimu kutokana na kukosa
elimu ya umuhimu na faida za takwimu.
“Jamii inapopewa taarifa za ukusanyaji wa takwimu iwe ya mifugo au
miti hujenga hofu, kwamba huwenda wanataka kutoleshwa kodi hapo
baadae’’,alishauri.
Hata hivyo washirikia hao, waliwashauri watumiaji wa takwimu wasisite
kuhakikisha kuitumia ofisi ya mtakwimu mkuu wa serikali, ili
kuhakikisha wanapata takwimu sahihi kwa matumizi ya shughuli zao mbali
mbali.
Katika semina hiyo ya siku mbili, mada kadhaa zilijadiliwa ikiwa ni
pamoja na sheria ya takwimu, umuhimu wa takwimu, takwimu za kiuchumi
pamoja na takwimu za kijamii, ambapo washiriki wa ni wafanyabiashara,
asasi za kiraia pamoja na watendaji wa serikali.
chanzo:zanzibar24.
Comments