Mtu mmoja
amefariki dunia na wengine sita hawajulikani walipo baada ya boti iliyokuwa
ikitokea Mombasa, kuelekea Wete, Pemba kupigwa wimbi kali na kuzama usiku
wa kuamkia leo.
Mkuu wa Wilaya
ya Wete, Rashid Hadidi alisema watu wengine kumi waliookolewa wamepelekwa
hospitali ya Wilaya ya Wete, kwa ajili ya matibabu.
“Boti hiyo ya Al
Hussein ilizama wakati ikishusha watu karibu na kisiwa cha Oesha na watu kumi
waliookolewa wamelazwa katika hospitali ya Wete,” alisema Hadidi.
Alisema idadi ya watu waliokuwamo katika boti hiyo ni 27, ambapo kumi ndiyo
waliookolewa.
Alisema aliyefariki ni raia wa Mombasa Kenya na bado jina lake halijapatikana.
chanzo:Mwanchi.
Comments