Mimba za utotoni ni janga la kitaifa zanzibar.

Wanafunzi wa Skuli ya Mpapa Sekondari   wameiyomba serikali kuendeleza juhudi za kutoa elimu ya kiraia maskulini  ambayo itaweza  kuwahamasisha  katika masuala ya udhalilishaji  na kuwaepusha na mimba za utotoni.
Wakizungumza katika mkutano maalumu ulioandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa
wamesema  mimba za utoto na ndoa za mapeme kuongezeka katika skuli yao  imesababishwa na tamaa na kuiga tamaduni za watu wengine  jambo linalowakatisha ndoto zao za maisha.
Nao walimu wa Skuli hiyo wamesema hali bado mbaya kimesababisha kiwango cha ufaulu kushuka  kutokana na  matatizo hayo na  wazazi wanachangia  kutokana na  ushirikiano  mdogo kwa  walimu katika malezi jambo linalosababisha   wanafunzi  kuolewa katika umri mdogo kutokana na tamaa za mali au kupata mimba za utotoni.
Kwa upande wake Afisa Ustawi  wa  Jamii Zanzibar  Mabula Nalimi amesema kutokana na kuongezeka kwa kesi za udhalilishaji ikiwemo ndoa za umri mdogo,mimba za mapeme , Serikali imeamua  kuanzisha mpango kazi wa kutoa elimu maskulini  ili kupunguza idadi kubwa ya kesi kwa kupatiwa hukumu pindi zitakapo jitokeza na hatofumbiwa mtu macho ili kunusuru taifa.
Mafunzo hayo yanalenga  kuwashajihisha watoto chini ya umri wa miaka 17 ili kuondokana na udhalilishaji.
chanzo:zanzibar24.

Comments