
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makondaamekabidhiwa ekari 1500 na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vigogo Nchini.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo amesema wameamua kumkabidhi eneo hilo ili kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda na kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.
Kwa upande wake RC Makonda ameeleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji, utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika na wilaya zote.
Pia RC huyo alisema mkoa wa Dar es Salaam unajengwa na wana Dar es Salaam wenyewe hivyo kama kuna watu wanataka kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Dar es Salaam wafanye hivyo.
Comments