
Watu mashuhuri walioanza kufungua listi hiyo mpya ni pamoja na Mbunge wa Hai Freeman Aikaely Mbowe,
mfanyabiashara mkubwa nchini, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima wametajwa kwenye orodha ya pili ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Makonda amewataja pia mbunge wa zamani wa Kinondoni wa tiketi ya CCM, Iddi Azan na mfanyabiashara maarufu wa nguo Jijini Dar es Salaam, Hussein Pambakali kwenye orodha hiyo ambayo ina watu 65.
Amesema orodha hiyo kwa upande wa vigogo wanahusishwa na biashara hiyo haramu na wengine wanatarajiwa kutoa taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo.
Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu.
Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.
chanzo:zanzibar24.
Comments