
Hayo yalisemwa juzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokuwa katika semina ya Masheikh, Wanazuioni, Maimamu na Walimu wa Quran Tanzania kupitia Jumuiya ya Walimu Wanaosomesha Quran Tanzania (JAWAQUTA).
Makonda alisema waumini hao 12 waliandaa mbuzi mweupe ili kumtoa kafara na yeye alifanikiwa kuwatambua kupitia mtandao wake.
Aidha, alisema kuwa haamini kama waumini hao ni wa dini ya Kiisalmu, bali kundi la watu waliokuwa wamevalia kanzu kwa utambulisho huo na kwamba huenda walitumika kuwalia watu fedha zao.
Katika semina hiyo, Makonda aliwataka viongozi wa dini kuendelea kutoa ushirikiano katika vita dhidi ya dawa za kulevya huku wakizidi kuwaombea viongozi wote kwa vita hii ni ngumu. Siku tutakapofika mbinguni, Mungu atatuuliza mamlaka haya aliyotupa hapa duniani tuliyatumiaje? alisema Makonda.
chanzo:zanzibar24.
Comments