Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua
uamuzi uliotolewa na Jaji kutoka mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita
alizizuia sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.
Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika Mahakama ya juu.
Na
muda mfupi tu baada ya Uamuzi huo wa mahakama kutangazwa, Rais Donald
Trum aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake
ataibuka mshindi.
''Ni
uamuzi wa kisiasa na tutaenda kukutana mahakamani. Na natarajia kufanya
hivyo, Tuna hali ambayo usalama wa nchi yetu uko hatarini na ni hali
mbaya sana..'' Alisema Trump.
Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza
mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu.
Akizungumza
wakati wav kuapishwa kwa Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Rais wa Marekani
amesema uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake
utalishughulikia suala hilo kuamzia sasa.
chanzo:bbc.
Comments