Chama tawala kilihesabu magari hayo mwezi mmoja kabla ya kuingia madarakani baada ya kupata ushindi uchaguzini mwezi Desemba.
Imekuwa
kawaida kwa baadhi ya maafisa wa serikali inayoondoka kutorejesha
magari ya serikali, na hulazimu serikali mpya kuyatwaa kwa nguvu nchini
Ghama.
Waziri mmoja katika serikali iliyoondoka ya John Mahama
hata hivyo amesema kuenezwa kwa habari kwamba wenzake walitekeleza
uhalifu ni makosa.
Aliyekuwa waziri wa usalama Omane Boamah ameambia mwandishi wa
BBC Thomas Naadi kwamba hiyo ni "mbinu inayotumiwa na serikali mpya
kuipa sababu za kununua magari mapya."
Msemaji wa rais Eugene Arhin aliambia wanahabari kwamba maafisa wa serikali mpya walipata magari:
Kituo
cha redio cha Citi FM nchini Ghana kimeripoti kwamba rais amelazimika
kutumia gari aina ya BMW lililoundwa miaka 10 iliyopita kutokana na
kutorejeshwa kwa magari hayo.
Alipokuwa anatoa taarifa yake, Bw Arhin alifichua kwamba afisi ya
rais ilifaa kuwa na magari zaidi ya 300 lakini hakueleza magari hayo
hutumiwa vipi.
Nana Akufo-Addo wa chama cha New Patriotic Party
alishinda uchaguzi mkuu mwanzoni mwa Desemba na kuchukua hatamu kutoka
kwa John Mahama, wa chama cha National Democratic Congress.
chanzo:bbc.
Comments