
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayubu
Mohammed Mahmud wakati akizungumza na waandishi wa habari akitangaza
rasmi juu ya mapambano ya utumiaji wa dawa hizo katika Mkoa wake na
Zanzibar kwa ujumla.
Amesema katika uchunguzi uliofanyika kumegundulika kuwa baadhi ya
watumishi ambao wamekua wakijihusisha na vitendo hivyo wakiwemo askari
wa jeshi la polisi 15 wanaotuhumiwa hivyo amehakikisha kupigana na
vitendo hivyo ili kuhakikisha biashara hiyo inatoweka Zanzibar.
Aidha amesema kuendelea kufanyika kwa biashara hiyo haramu kumeweza
kusababisha athari nyingi kwa vijana ikiwemo kuongezeka kwa uhalifu na
kupunguza uzalishaji mali ndani ya nchi ambao una mchango mkubwa
katika kuinua uchumi.
Kwa upande wake kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za
Kulevya Tanzania Rogers William Sianga amesema kazi ya kupambana na
utumiaji wa dawa za kulevya si ya Tanzania bara peke yake bali ni ya
nchi nzima na watahakikisha wanapambana ili kutokomeza biashara hiyo.
Zaidi ya maduka 16 yamegundulika kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya katika mkoa wa mjini magharibi.
chanzo: Zanzibar24
Comments