Waziri Mkuu
mstaafu na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kesho (Jumamosi)
atakuwa miongoni mwa maelfu ya washabiki watakaoudhuria mechi ya watani wa
jadi, Simba na Yanga itakayochezwa uwanja wa Taifa jijini hapa.
"Kesho
nakwenda uwanjani, usitake kujua mimi ni mshabiki wa timu gani, subiri
utaniona uwanjani" amesema Lowassa ambaye hajawahi kuweka wazi ni
mshabiki wa timu gani, zaidi ya kusema anaipenda Manchester United.
Lowassa amesema
kinachomsukuma zaidi kwenda uwanjani ni kuungana na wadau wa soka nchini na
kujionea ambavyo ligi ya Tanzania inavyokuwa na msisimko kama ilivyo kwa ligi
za nje.
"Nasikitika
ninapoona watu tunazipenda sana timu za nje.Yale mahaba ya zamani kwa timu zetu
yako wapi?michezo hususani mpira ni eneo pana sana la ajira kwa vijana
wetu," amesema Lowassa ambaye alikuwa mchezaji wa mpira wa kikapu hapo
zamani.
chanzo:Mwananchi.
Comments