Thomas Nahimana ambaye ni
kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa ametangaza kuunda serikali
hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni.
Katika mazungumzo na BBC,
mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani
serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza
wananchi.
Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha
kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa
kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Baadhi ya aliowataja katika baraza lake la mawaziri ni wafungwa
wanaotumukia vifungo vya jela nchini Rwanda kwa makosa kama vile
kukanusha kuwa mauwaji ya kimbari hayakufanyika nchini Rwanda mwaka
1994.
Bw Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.
chanzo:Bbc.
Comments