Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe......Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo..

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Pia Sirro ameamuru watu wote waondoke kituoni hapo.
"Oparesheni ya dawa za kulevya bado inaendelea na kuanzia sasa hatutaruhusu mkusanyiko wa wananchi karibu na kituo cha polisi hiki watakaoonekana watashughulikiwa na asije akalaumiwa Kamishina Sirro kwa kuwa tayari nimeshatoa taarifa."
chanzo:mpekuziblog.
Comments