Khatib Mohammed Khatib miaka 58 leo ametiwa hatiani na mahakama ya wilaya ya kusini Unguja kwa kosa la kumtorosha msichana mwenye umri wa miaka 14 aliye chini ya uangalizi wa wazazi wake.
Hakimu Ali Abdurahman wa mahakama hiyo amefikia uamuzi huo na kumtaka mshtakiwa kutumikia chuo cha mafunzo miaka mitatu 3 kama inavyo elezwa nakifungu cha 130 (A) cha sheria namba 6 ya mwaka 2011.
Sambamba na hilo mshtakiwa huyo ametakiwa kulipa fidia ya madhara aliyomsababishia muathirika wa tukio hilo shilingi laki tano au kuendelea nakifungo cha miezi 6.
Waendesha mashtaka Ali Yussuf Ali na Suleiman Yussuf Ali waliiyomba mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshtakiwa ili iwefundishokwa wengine hasa hasa ikizingatiwa kuwa kesi nyingi zinazoripotiwa katika ukanda huo kuhusisha watu wazima wa umri wa khatib ambao wapaswa kuwa walinzi wa watoto hao.
Kundi la wanaharakati kutoka mitandao ya wanawake na watoto wa wilaya hiyo na watendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA ofisi ya Zanzibar waliliambia jopo la waandishi wa habari lililokua likifuatilia kesi hiyo kua wameridhika na hukumu hiyo ambayo walidai ni matokeo ya kutolewa kwa elimu ya mara kwa mara ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wakijinsia.
Hiyo nikesi yakwanza ya udhalilishaji wakijinsia kati ya saba (7) zilizo simamiwa na ofisi yamkurugenzi mashtaka wa serikali ya Zanzibar (DPP) kupatiwa hukumu toka oficsi hiyo ilipo anzishwa rasmi mwezi septemba, 2016.
chanzo:zanzibar24.
Comments