Hukumu ya kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwanasheria Mkuu kusomwa Machi 8.

jamii
Hukumu ya kesi ya Jamii Media dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Jeshi la Polisi kuhusu matumizi mabaya ya Sheria ya Makosa ya Mtandao kusomwa tarehe 8 Machi.



Hukumu hiyo itasomwa Mahakama Kuu, mbele ya Mtukufu Jaji Kitusi baada ya kushindikana kusomwa tarehe 22 Februari.



Kampuni ya Jamii Media ambao ni waendeshaji wa mtandao wa JamiiForums na FikraPevu walifungua kesi ya Kikatiba kutaka vifungu vya 32 na 38 vya Sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya.



Kwa kudai yakwamba Vifungu hivyo vinavunja haki za msingi za Watanzania watumiao mitandao kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

chanzo:zanzibar24.

Comments