
Kasi kubwa ya uchimbwaji wa mchanga katika vitalu tofauti vya
rasilmali hiyo ili kukidhi mahitaji hayo ya ujenzi imepelekea Serikali Kuu
kusitisha zoezi hilo kwa muda ili kukamilisha utaratibu sahihi kutokana na
athari kubwa iliyokwisha jitokeza kwenye maeneo yaliyochimbwa mchanga.
Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiiongoza Timu ya Mawaziri,
Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu pamoja na Wataalamu wa Taasisi zinazosimamia
mazingira, misitu na Ardhi walifanya ziara maalum ya kutembelea maeneo
yaliyokwisha athirika na kadhia hiyo.
Ziara
hiyo ilijumuisha pia maeneo ya ardhi ya Donge Kipange, Donge Mchangani, Donge
chechele na Pangatupu ambayo wamiliki wake binafsi wameshapeleka maombi yao
kwa ajili ya kuruhusiwa kuchimba mchanga ili kukidhi mahitaji yao ya
kimaisha.

Ndugu
Juma alisemaTimu ya Makatibu Wakuu iliyopewa jukumu la kufanya utafiti wa
kuelewa maeneo yaliyoathirika na yaliyobaki kwa kushirikisha wataalamu wa
Masuala ya Mazingira, Misitu na Ardhi imethibitisha kwamba hivi sasa zipo hekta
137 pekee zilizobakia kwa ajili ya kuchimbwa mchanga katika kisiwa cha Unguja
zilizopo katika Kijiji cha Pangatupu.
Alisema
timu hiyo hivi sasa inakamilisha ripoti ya utafiti huo na kutoa ushauri pamoja
na mapendekezo na baadae kuyapeleka Serikalini kwa lengo la kuchukuliwa
hatua zitakazofaa kufuatwa hapo baadae.
Naye Mkurugenzi wa
Idara ya Ardhi na Usajili Zanzibar Nd. Said Salim Afuso alisema
maeneo mengi yaliyochimbwa mchanga yangeweza kurejea katika uhalisia wake
ndani ya miaka miwili iwapo uchimbaji uliofanywa kabla ungezingatia Kanuni za
Mazingira.

Mkurugenzi
huyo wa Idara ya Ardhi na Usajili alifafanua kwamba maeneo yote ya Ardhi
yaliyomo ndani ya Visiwa vya Zanzibar tayari yameshapimwa na kuwekewa
utaratibu wa matumizi kulingana na hali halisi iliyopo ya mazingira.
Hata
hivyo ameeleza kwamba baadhi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli
za kuendeleza Kilimo yameshavamiwa kwa harakati za ujenzi wa makaazi ya
kudumu na mengine kuchimbwa mchanga.
Kwa upande wao
Wananchi wanaomiliki maeneo yanayotaka kuchimbwa mchanga wakisubiri kupata
kibali kufuatia maombi waliyopeleka wameieleza Timu hiyo ya Viongozi Wakuu
kwamba wamefikia hatua hiyo baada ya maeneo yao kukosa sifa za kuyaendeleza kwa
shughuli za Kilimo.

chanzo:zanzibar24.
Comments