
Akizungumza na wanachama wa CCM katika ziara maalumu iliyofanyika
katika tawi la Mwembeladu Jimbo la Rahaleo Naibu katibu Mkuu CCM Vuai
Ali Vuai amesema kuna baadhi ya watu wanaitumia vibaya mitandao ya
kijamii kwa njia ya kuwachafua viongozi wajuu wa chama na kuwapotosha
wanaccm kwa lengo la kukivuruga chama.
Hata hivyo amewataka viongozi wa CCM kuwacha tabia ya kuchafuana
kwa njia za mitandao ya kijamii jambo ambalo linatia doa chama na
kupelekea kukiyumbisha chama hivyo amesema kutokana na matatizo
hayo yanayofanywa kwa makusudi chama kitawaajibisha kupitia kamati
ya maadili ya uongozi ili kulikomesha jambo hilo.
Aidha ametoa wito kwa wanachama wa chama cha mapinduzi
kutoyazingatia maneno yanayosambazwa katika mitandao na wapimzani
kuwa ccm itatoka madarakani.
chanzo:Zanzibar24
Comments