Akizungumza katika kongamano la kuadhimisha miaka 40 ya ccm huko Meli nne saccos amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia ccm lakini bado kuna watu wanakipa vikwazo chama katika
hatua zake za kusonga mbele na kutaka kukiangusha lakini tathimini itayofanywa kwa uadilifu itawabainisha watu hao bila ya woga.
hatua zake za kusonga mbele na kutaka kukiangusha lakini tathimini itayofanywa kwa uadilifu itawabainisha watu hao bila ya woga.
Hata hivyo amesema wakati umewadia kwa chama kufanya tathimini kuanzia ngazi ya tawi, mkoa hadi taifa ili kuangalia changamoto zinazosababisha matabaka na makundi hayo yasioleta faida katika chama na amesema ili kukijenga chama imara lazima wanachama wawe wamoja,wakweli,waadilifu kwalengo la kukivusha chama katika siasa za mivutano.
Aidha Balozi Seif amewataka viongozi mbalimbali katika chama na serikali kuwacha tabia ya kujigawa matabaka na makundi ambayo haya tija katika chama na badala yake kufanya kazi kwa mashirikiano na kwa uwadilifu ili kuwaletea wananchi maendeleo yatakayoweza kuwanufaisha katika jamii.
chanzo:zanzibar24.
Comments