Bombardier Q400 yashindwa kuruka kutokana na hitilafu.

atcl bombardier q400Jijini Mwanza, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Bombardier Q400 ilishindwa kuruka kutoka uwanjani hapo kutokana na kupata hitilafu.

Katika uwanja wa ndege wa Mwanza, abiria wa ndege ya Bombardier walishindwa kufanya safari yao ya kuelekea jijini Dar es salaam kutokana na ndege waliyokuwa waitumie kupata hitilafu. 

Ndege hiyo yenye namba 5H-TCB ilitakiwa kuruka kutoka Mwanza saa moja kamili jioni lakini ilishindwa.

“Mara ya kwanza ndege iliruka baadae ikatua, ikaruka tena kwa mara ya pili na baadae ikatua, ndipo mmoja wa wahudumu akatangaza tushuke ili waikague ndege hiyo kwani ilionesha kuna tatizo,” alisema abiria mmoja. 

Alisema iliwalazimu kubaki uwanjani mpaka saa saba kasorobo usiku wakisubiri ndege nyengine ya kampuni hiyo iliyokuja kuwachukua na kufika Dar es salaam saa nane usiku.

chanzo: zanzibar24.

Comments