Ibrahim Rahimpoor, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran anayehusika na masuala ya Asia na Ocenia jana alimuita Reza Hakan Tekin balozi wa Uturuki hapa mjini Tehran na kumkabidhi rasmi malalamiko
ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na matamshi yaliyotolewa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na waziri wake wa mashauri ya kigeni Mevlüt Çavuşoğlu dhidi ya taifa hili.
Akihutubia siku ya Jumapili katika mkutano wa usalama wa Munich Ujerumani, Mevlüt Çavuşoğlu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki alidai kwamba, Iran inafanya njama za kuzifanya nchi mbili za Iraq na Syria ziwe za Kishia.
Aidha wiki moja kabla yake, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki akihutubia katika taasisi ya kimataifa ya amani huko Bahrain alitoa tuhuma dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Erdogan aliashiria migogoro ya Mashariki ya Kati kama ya Syria na Iraq na kudai kwamba, katika nchi hizo kwa wakati mmoja kuna mjadala na mvutano wa kikaumu na kimadhehebu.
chanzo:parstoday.
Comments