Akizungumza na vyombo vya habari mjini Beirut, Zasypkin amesisitiza kuwa kipindi cha hivi sasa ni hasasi na muhimu; na nchi zote zinapaswa kutoa ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi.
Balozi wa Russia nchini Lebanon ameashiria msimamo wa nchi yake kuhusu Syria na kueleza kwamba msimamo wa kistratijia wa Russia nchini Syria wa kutokea miaka ya huko nyuma hadi sasa haujabadilika na kwamba tangu ulipoanza mgogoro wa nchi hiyo Moscow imekuwa ikitaka iandaliwe ramani ya njia ya kisiasa kwa ajili ya kuutatua mgogoro wa Syria kwa njia za amani.
Alexander Zasypkin, aidha ameongeza kuwa Russia ina hakika kwamba uchaguzi wa bunge utafanyika nchini Lebanon; na Moscow inayapa umuhimu makubaliano yaliyofikiwa baina ya vyama na mirengo ya kisiasa kuhusu sheria za uchaguzi wa nchi hiyo.
Mbali na msimamo uliotangazwa na Russia kuhusu Hizbullah, rais mpya wa Lebanon Michel Aoun naye pia alitangaza hapo kabla kuwa Hizbullah ni harakati inayodhamini ulinzi wa nchi hiyo.
chanzo;parstoday.
Comments