
Alisema Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umekwisha kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na kuwataka kuelekeza nguvu zao katika kusimamia miradi yao ya maendeleo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akitoa salamu kwenye Hafla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu za Soka zitakazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo hapo ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Aliwatanabahisha wale wote wanaoendeleza kasumba ndani ya mitandao ya Kijamii kwa kuwadanganya Wananchi kwa makusudi waendelee kuvumilia na kustahamili hadi utakapofika uchaguzi mwengine Mkuu wa Mwaka 2020.

chanzo:zanzibar24.
Comments