Kauli hiyo imetolewa na Balozi Mstaafu wa Tanzania ambae kwa sasa amekuwa mhadhiri wa Elimu ya Chuo Kikuu
Nchini Balozi Msuya Waldi Mangachi wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Ofisi za Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Msuya Waldi Mangachi ambae katika mazungumzo hayo alimkabidhi nakala ya Kitabu alichokitunga kinachoelezea uzoefu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya zamani alisema mgawanyo wa fursa hizo utakaokuwa na muelekeo wa kutumia maeneo yote utasaidia kuondoa au kupunguza malalamiko yanayoweza kuonyesha sura ya upendeleo wa upande mmoja.
Balozi Msuya alisema sababu za msingi zilizopelekea kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki mnamo mwaka 1977 ilitokana na mitizamo tofauti ya kisiasa na hasa falsafa ya kujenga uchumi baina ya Nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
Mtaalamu huyo wa Fani ya Udaktari wa Historia alieleza kwamba Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya zamani isingeweza kufanikiwa bila ya kubadilika kwa mfumo wa uchumi Kimataifa.
Alisema mfumo uliotumika ulizikuta Nchini wanachama zikizalisha malighafi na kuziuza kwa nchi za Kaskazini na matokeo yake wanunuzi hao walichakachua malighafi hiyo na kuzirejesha kwa wazalishaji hao kama bidhaa za Viwandani.
Balozi Msuya alifafanua kwamba mantiki ya ushirikiano uliopo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki bado haijakaa vizuri licha ya kwamba biashara huru ndio njia pekee ya kuimarisha ushirikiano wa Jumuiya yoyote ile iwe ya Nchi au ya kanda.

chanzo:zanzibar24.
Comments