Shirika hilo limesema viongozi hao
wanaendeleza kile inachokitaja kuwa kuwatumia vibaya wakimbizi, kwa
manufaa yao ya kisiasa, badala ya kutanzua kiini hasa kilichowafanya
wakimbizi hao kuyakimbia mataifa yao.
Katika ripoti yake ya kila mwaka, Amnesty inaelezea mwaka 2016,
kama mwaka wa matamshi yaliyojaa chuki huku hofu ikapanda zaidi na
kufikia kiwango ambacho hakijawahi kufikia tangu miaka ya 1930, wakati
Adolf Hitler, alipoingia uongozini nchini Ujerumani.
Ripoti hiyo inapinga sera ambazo zinakubalia ubaguzi wa rangi na chuki.
Inasema
mataifa mbalimbali duniani yanaendesha ajenda potovu ambayo inawahujumu
wakimbizi ambao wanashutumiwa kwa makosa ambayo hawakutenda huku pia
wakidhulumiwa kijumla.
chanzo:bbc.
Comments