Aliyepanda zao la bangi nyumbani kwake atiwa mikononi mwa polisi.

Zanzibar kumekua na ulimwaji wa mazao mengi sana lakina kijana mmoja aitolea nyumba yake sadaka na kulima zao la bangi jambo ambalo ni la kushangaza kwa upande wa Zanzibar na ni kosa kisheria.
Tukio hilo la kulimwa bangi zanzibar lililofanywa na kijana aliyetambulika kwa jina la Hassan Ali Hassan maarufu robo mkaazi wa
 Bububu Kihinani Wilaya Magharibi Unguja limewashangaza na kuwashtua zaidi wakaazi wa eneo hilo.
Kufuatiwa kuwepo kwa hali hiyo askari polisi kituo cha Bububu wakishirikiana na kikundi cha ulinzi shirikishi shehia ya Kihinani wavamia nyumba hiyo na zana mbali mbali za kungolea bangi hiyo huku mmliki wa shamba hilo atimua mbio pasipojulikana.
Nao wakaazi wa maeneo hayo hilo wameshituswa sana na tukio hilo na kulitaka jeshi la polisi kutembelea mara kwa mara eneo hilo ili kunusuru watoto wanaoishi maeneo hayo kuathirika na zao hilo.
chanzo:zanzibar24.

Comments