Zitto alitoa kauli hiyo Ijumaa hii katika mkutano wa hadhara wa
kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Nkome mkoani Geita kupitia
ACT-Wazalendo.
“Hali ya chakula nchini si nzuri. Wananchi mmeshuhudia namna bei za
vyakula zinavyopanda kila siku. Bei ya sembe sasa kilo moja imefikia
shilingi 1,600 pale Morogoro, kilo moja ya mchele ni shilingi 1,500,
maana yake leo ugali na wali imekuwa bei inafanana. Gharama za maisha
zitaendelea kupanda kutokana na uhaba wa chakula kuwa mkubwa”.
“Ninapendekeza serikali hatua muhimu ya kisheria ya kutangaza balaa
la njaa nchini, tamko la balaa la njaa nchini litaisaidia serikali
kupata bajeti ya dharula ya kununua chakula na kutoa uhuru kwa wakuu wa
wilaya kutangaza maeneo yao kuwa yana njaa” .
Hivi karibuni Waziri wa kilimo, Charles Tizeba, walitofautiana na
Zitto kuhusu hali ya chakula ambapo waziri huyo alisema hali ya chakula
nchini ni shwari huku mbunge huyo wa Kigoma akisema ni mbaya.
chanzo: zanzibar24
Comments