Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amezindua maabara ya somo la Hisabati.
Akizindua maabara hiyo jijini Dar es Salaam, Waziri huyo amesema mpango huo utasaidia kujenga msingi mzuri wa somo la Hisabati kwa wanafunzi.
“Kama tunavyojua watoto wetu wanapenda mambo ya teknolojia, unakuta mara nyingi wako kwenye simu wako kwenye komputa kwahiyo ni mfumo ambao unaendana na vitu ambavyo vinawavutia vijana. Ni dhahiri kwamba kama una vutiwa na kitu uwezekano wa kukifanya vizuri ni mkubwa kuliko jambo ambalo halikuvutii,’ alisema Ndalichako.
chanzo:zanzibar24.
Comments