Watoto hao wamebainika kupururuka kuanzia hata ngazi ya nne
wanaposhuka chini na wakati mwengine wakiwa zaidi ya watatu jambo ambalo
linaweza kusababisha maafa pindi wakianguka.
Wazkiungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti majirani
wa nyumba hizo, wamesema imekuwa ni mtindo kwa watoto wanaoishi nyumba
hizo kujihatarishia maisha yao.
Amina Khamis Makame wa Mtemani Wete, alisema mtendo huo zaidi
hufanywa kati za usiku au kwa siku za mapunziko wanapokua hawakwenda
chuoni au skuli.
“Hupururuka kwa kutumia makalio yao kutoka ngazi ya nne hadi ya
chini, na wakati mwengine huwa zaidi ya watatu, ni hatari maana akikosa
mtelezo anaweza kuanguka’’,alifafanua.
Nae Mwanahija Kombo Omari wa eneo hilo, alisema lazima wazazi wa
watoto hao, wajiwekee mikakati ya kuwazuia watoto hao kabla halijatokeza
kubwa.
Kwa upande wake Said Khamis Juma wa Madungu Chakechake, alilizishauri
kamati za sheha kuwaita wakaazi wa nyumba hizo ili kuwapa habari za
watoto wao.
Mwadini Ali Mchama ‘bamcha’ alisema imekuwa ni kwaida hata kwa watoto
wasioishi nyumba hizo za maendeleo kufanya mchezo wa kuteleza kwenye
mgomgo wa ngazi hizo.
Mmoja wa wazazi wanaoishi kwenye nyumba hizo za maendelo za Madungu
aliejitambulisha kwa jina moja la Salum, alisema imekuwa vigumu kuwazuia
watoto wa familia nyengine.
“Mwandishi miaka hii kila mmoja analea mwanawe, wangu hawaingia
kwenye mchezo, huu lakini wa wenzangu wasiokatazika
wanaendelea’’,alifafanua.
Nae mzazi Hassina Mjaka Mathias wa Mtemani Wete, alisema ghorofa
analoishi yeye kwa mwaka mmoja sasa wamefanikiwa kuwazuia watoto na hasa
baada ya kutokezea mmoja wao kuanguka.
“Alikuja mtoto kwangu kuja kutembea, wakati anafanya mtelezo huo
aliangua ngazi wa chini na kuumia ndio maana wazazi tulikutana na kupiga
marufuku’’,alifafanua.
Mtoto Himid Salum anasema kwa sasa mchezo huo wameuawacha, ingawa wanaofanya ni wenzao wasioishi kwenye nyumba hizo.
“Wanaofanya ni watoto wale wanaokuja mara moja kwa kutumwa kwenye
nyumba hizi za ghorofa, lakini sisi tumeshaacha mchezo huo wa
kutekeleza’’,alifafanua.
Sheha wa shehia ya Mtemani, Mrisho Juma Mtwana alisema alishapiga
marufuku kwa muda mrefu juu ya mchezo huo kwa kushirkiana na wazazi
husika.
“Nashukuru tumefanikiwa kuuzima mchezo wa kuteleza, ambao
ulishashashiika kasi, lakini sasa twashukuru baada ya kukutana na wazazi
hakuna tena michezo hiyo’’.alifafanua.
Katika miaka ya hivi karibuni watoto wanaoishi na wasioishi kwenye
nyumba za maendeleo wamekuwa wakiendesha mchezo wa kuteleza kwa kutumia
kuza za vidaraja vilivyomo kwenye nyumba hizo.
chanzo: zanzibar24.
Comments