Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mohammed Aboud wakati akifungua kikao cha mawaziri wa pande
mbili pamoja na makatibu wakuu na watendaji.
Alisema nia ya serikali zote mbili ni kuona kero zilizopo katika
Muungano zinatatuliwa haraka ili wananchi wazidi kufaidi matunda ya
Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu zaidi ya miaka 53 sasa.
Aboud alisema kufanyika kwa vikao hivyo ni muendelezo wa utekelezaji
wa maagizo ya viongozi wakuu ambao wanasisitiza kupatiwa kwa ufumbuzi wa
haraka wa kero za Muungano.
Mapema akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamo wa rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Januari Makamba
alisema hicho ni kikao cha nane tangu kuundwa kwa kamati ya pamoja ya
kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano mwaka 2008.
Alisema maagizo ya viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais John Magufuli
na Rais Ali Mohamed Shein ni kuona kero zote zilizomo katika Muungano
zinapatiwa ufumbuzi ili wananchi waweze kufaidika na matunda ya
Muungano.
Makamba alisema wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukitimiza
umri wa miaka 53 mafanikio makubwa yamepatikana kwa wananchi wa pande
zote huku kero nyingi zilizokuwepo awali zikipatiwa ufumbuzi haraka.
Ofisa mmoja mwandamizi kutoka wizara ya fedha na mipango ya serikali
ya Zanzibar alisema baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ambayo bado ni
kikwazo ni suala la kodi kwa pande mbili ikiwemo uingizaji wa bidhaa.
Kikao hicho kinatazamiwa kupata baraka za waziri mkuu wa Kassim Majaliwa
pamoja na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.
chanzo;habarileo.
Comments